Wajibu Wa ma-Khatwiyb Kwa Wanaoingia Siku Ya Ijumaa Na Kukaa


Swali: Ni wajibu kwa ma-Khatwiyb wote siku ya Ijumaa kuwaamrisha wale wanaoingia na kukaa kuswali Rakaa mbili [za Tahiyyat-ul-Masjid]?

Jibu: Nido, bila ya shaka. Awazindue watu na kuwafunza ya kwamba haijuzu kukaa. Anayeingia na Imamu anatoa Khutbah haijuzu kwake kukaa mpaka aswali Rakaa mbili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1430-5-29.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014