Wajibu wa kumuamsha mke katika swalah ya Fajr


Swali: Ninamuamsha mke wangu katika swalah ya Fajr lakini anachelewa kuamka. Mara nyingi haswali swalah ya Fajr isipokuwa katika wakati wa mwisho. Je, wajibu wangu ili kujitoa katika dhimma yangu ni kule kumuamsha tu au ni wajibu kwangu kusimama juu yake mpaka aamke?

Jibu: Ndio. Ni lazima. Haitoshelezi kuamrisha tu. Mlazimishe juu ya swalah. Haitoshelezi kumwambia tu “Swali” ukaenda zako na kumwacha. Ni lazima uhakikishe hukutoka mbele yake isipokuwa ameamka na ameingia katika swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mntq--20041434.mp3
  • Imechapishwa: 19/09/2020