Wajibu wa kila Salafiy kabla ya kuanza kulingania


Swali: Ni kitu gani ambacho ni wajibu kwa Daa´iy (mlinganiaji) ambaye ni Salafiy kuanza nacho?

Jibu: Ni wajibu kwanza kwake kuanza na nafsi yake mwenyewe na apange wakati wake kuihifadhi Qur-aan, kusoma kitu katika vitabu vya lugha ya kiarabu ikiwa yuko na mwenye kumfunza. Hali kadhalika al-Mustwalah ikiwa yuko na mwenye kumfunza. Hali kadhalika aipe umuhimu ´Aqiydah; kwa mfano wa al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, Kitaab-ut-Tawhiyd cha Ibn Khuzaymah na as-Sunnah cha Ibn Abiy ´Aaswim. Ni lazima aupange vizuri muda wake na ajitayarishe kuwa mtoa mawaidha, Khatwiyb, mhakiki na mwalimu. Ili aweze kupiga Radd makundi yote. Haitoshi kwake kuhifadhi kisa cha mvulana na mchawi au akahifadhi mlango katika Riyaadh-us-Swaalihiyn halafu akawa anahama kutoka kwenye Msikiti huyu na kwenda Msikiti mwingine. Hili ni jambo ambalo anapewa thawabu kwalo. Lakini sisi tunachotaka ni awe bora kuliko hivyo na awe kama inavyosemekana. Awe kama mithali isemayo: “Awe ni mwanaume mwenye miguu ardhini. Na hamu yake kubwa iko kati ya nyota.” Ni jambo muhimu aanze kwa ´Aqiydah. Ajifunze na kusafiri kwenda kwa wanachuoni ikiwa hakuna yeyote katika mji huyo. Ni juu yake asafiri kwenda kwa wanachuoni na aitoe nafsi yake kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jalla).

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=7596
  • Imechapishwa: 10/03/2018