Wajibu kwa wazazi wenye uwezo kuwaoza watoto wao


Wazazi wamche Allaah (´Azza wa Jall). Watambue kuwa wana uwajibu wa kuwaoza watoto wao midhali wako na uwezo. Ni wajibu kwao kuwaoza kama ambavyo ni wajibu kwao kuwalisha, kuwavisha na kuwapa makazi. Ni wajibu kwao vilevile kuwaoza. Hili ni kwa njia ya uwajibu. Watambue kuwa wasipofanya hivo ni wenye kutenda madhambi na ni mabakhili ambao wanafanyia ubakhili vile Allaah alivyowapa katika fadhila Zake huku wakidhani kuwa ni kheri kwao ilihali ni shari kwao.

Lau tutakadiria – namuomba Allaah asijaalie kuwa hivo – mtoto akaharibika kwa sababu baba yake amekataa kumuozesha na wakati huohuo akawa na uwezo juu ya hilo, basi mzazi wake huyo anapata madhambi kwa kuharibika huku. Kwa sababu yeye ndiye kasababisha.

Halafu jengine tunamwambia mzazi huyu: huenda ukaenda kulala na usiamke isipokuwa umefariki na mali zako zote zikaenda kwa mtoto huyu ambaye unambania. Hivyo mche Allaah! Utawaona wazazi wanasema kuwa hawawezi kuwaoza watoto wao kwa sababu wameshakuwa wanaume ambao wanaweza kujiolea wenyewe. Kutakasika kutokamana na mapungufu ni kwa Allaah! Je, wao wana uwezo wa kufanya hivo? Je, kila yule ambaye anamaliza masomo anapata kazi? Si kweli. Huenda akafanya mwezi, miezi miwili, mwaka au miaka miwili hajapata kazi. Jambo haliko mikononi mwao.

Kwa hivyo nasema kwamba mtu yeyote ambaye Allaah amemtajirisha na akawa na uwezo wa kumuoza mtoto wake na wakati huohuo mtoto akawa anamuomba hilo – ima moja kwa moja kwa kusema au kwa ishara – na baba akawa anakataa kufanya hivo, basi atambue kuwa anapata madhambi. Kwa sababu ameacha kufanya jambo la wajibu juu yake.

Ama kuhusu vijana nawausia kufanya subira, kutarajia thawabu kwa Allaah na kujichunga na machafu. Wakifanya hivo, basi Allaah atawasaidia katika fadhila Zake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/776
  • Imechapishwa: 10/01/2018