Waislamu wanaowapenda makafiri na kuonelea kuwa dini zote za kimbingu ni za haki


Swali: Tunapopata mihadhara kama hii na tukasikia maneno yako kuhusu manaswara na mayahudi basi imani yetu, kuwapenda kwetu waumini na kuwachukia kwetu maadui wetu na kujitenga kwetu mbali nao kunazidi kupanda. Lakini tunaona watoto wetu wanalelewa katika malezi yaliyo kinyume na hayo. Tunawaona waislamu wengi wanalelewa juu ya kuwapenda watu hao kupitia zile filamu wanazotazama kiasi cha kwamba akili inastaajabishwa mpaka akili za watoto wale zinafungamana na makafiri wale. Matokeo yake wakashangazwa nao na kuwaogopa. Unasemaje? Tufanye vipi ili kuuokoa Ummah wa Kiislamu na jambo kama hilo?

Jibu: Yaliyotajwa na muulizaji ni jambo la kihakika kweli. Kuna katika waislamu ambao hawajitengi mbali na washirikina. Hata kama watajitenga mbali kwa ndimi zao basi hawafanyi hivo kwa mioyo yao. Wanawapenda na wanawafanya marafiki. Allaah anasema katika Qur-aan tukufu:

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ

”Hutopata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanaompinga Allaah na Mtume Wake.”[1]

Ni vipi mtu atasema kuwa yeye ni mwenye kumuamini Allaah na kwamba anampenda Allaah ilihali anawapenda maadui wa Allaah?

Unawapenda maadui wa mpenzi na huku wadai kuwa unampenda!

hilo ni jambo lisilowezekana

Kila mtu ambaye anawapenda maadui wa Allaah sio mwenye kumpenda Allaah. Hili ni jambo lililo katika maumbile ya watu. Kila kiumbe ameumbwa katika maumbile haya. Tahadhari na jambo hili la kuwapenda maadui wa Allaah. Haijalishi kitu hata kama watabobea katika mambo ya elimu kama vile udaktari na mambo mengine yenye kuwanufaisha watu, bado wao watabaki kuwa ni maadui. Hawawezi hata siku moja kufanya hayo kwa manufaa ya waislamu. Bali wao wanafanya bidii kujaribu kuwafanya waislamu kuwa wadhaifu, kuwatawanyisha au kuwachana waislam. Wanafanya hivo ima kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja.

Kuhusu yale aliyoashiria katika yale yanayoonekana au kusikizwa katika mafilamu na kwamba watoto wamefungana nayo, hili ni janga kubwa. Ni wajibu kwa kila mtu ambaye anamcha na anaiogopa siku ya hesabu kuwalinda watoto wake kutokamana na hayo na awazuie kabisa kuangalia kitu kinachoitia kasoro ´Aqiydah. Vilevile awafanye wawachukie maadui wa Allaah kwa hali yoyote ile. Mtu ataulizwa siku ya Qiyaamah juu ya watoto na familia yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanaume ni mchungi juu ya familia yake na ataulizwa kwa kile alichokichunga.”

Vilevile anatakiwa kuwazuia kuangalia yale yanayoonekana katika baadhi ya magazeti machafu ambayo yanachukuliwa na watoto na kuyasoma. Matokeo yake nyoyo zao zinafungamana na watu hawa. Sambamba na hilo utamkuta muislamu huyo anawadharau waislamu na yale mambo yao ya dini wanayofanya.

[1] 58:22

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (30)
  • Imechapishwa: 10/10/2017