Waislamu wanaoritadi kila alfajiri kwa ajili ya kazi zao


Swali: Je, una nasaha kwa ambaye anaswali Fajr pindi anapotaka kwenda kazini baada ya kuisha wakati wake?

Jibu: Hii ni jarima kubwa mtu akaswali Fajr wakati anapoenda kazini. Jopo la wanachuoni wametoa fatwa kwamba anakuwa mwenye kuritadi ikiwa ndio mazowea yake kufanya hivo. Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz (Rahimahu Allah) na jopo la wanachuoni wametoa fatwa hiyo. Kwa sababu hakuswali swalah ndani ya wakati wake. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا

“Kwani hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.”[1]

Ambaye anaweka alamu ya saa moja juu ya kazi yake na wala haamki isipokuwa mara moja baada ya hiyo saa moja, jopo la wanachuoni wamefutu wamefutu kwamba anakuwa murtadi. Wanachuoni wengine wakasema kuwa jarima yake ni kubwa zaidi kuliko jarima ya mzinzi na mnywaji pombe ingawa hakufuru ukafiri mkubwa. Ambaye itampita kwa kutokusudia ni mwenye kupewa udhuru.

[1] 04:103

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191634
  • Imechapishwa: 17/04/2020