Waislamu leo kuwa madhalilifu – Sababu ni kupuuzia mfumo wa Salaf

Tunawanasihi vijana Salafiyyuun, na wale ambao walikuwa Salafiyyuun kisha wakaacha mfumo huu, watafute elimu na kusoma vitabu vya Salaf-us-Swaalih na wasidanganyike na vitabu vya waliokuja nyuma ambao hawana elimu juu ya mfumo wa Salaf na hawakusoma Uislamu sahihi na Sunnah. Wanaufafanua Uislamu bila ya elimu na hivyo wakawa wametumbukia katika makosa yanayohusiana na ´Aqiydah, Fiqh, fikira na siasa.

Enyi vijana! Ni lazima kwenu mjihimize na kutafuta elimu na kutilia umuhimu mfumo wa Salaf-us-Swaalih. Khaswa wale wa mwanzoni na halafu baada ya hapo mshuke kwa Ibn Taymiyyah na wanachuoni mfano wake miongoni mwa wanafunzi zake na wale waliopita njia yao katika wanachuoni wenye kulingania katika dini ya Allaah Saudi Arabia, Yemen, India na kwenginepo ambao wamepita njia ya Salaf-us-Swaalih.

Kujengea kwa haya mtaweza kuyatatua matatizo ya waislamu na kuwaondosha kwenye udhalili waliyomo. Hilo ni kutokamana na sababu ya ujinga na kupuuzia mfumo huu. Hilo vilevile ni kutokamana na vitabu vya wafikiriaji [Mufakkiriyn] waliokuja nyuma ambao hawakuwazidishia Waislamu jengine zaidi ya kupiga dinbwi kwenye ujinga na kuzidi kuwa mbali na mfumo huu wa Salafiyyah ambao ndio sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/HamadOthman/Divers/05Rabee01.mp3
  • Imechapishwa: 14/07/2020