Swali: Je, ni sahihi kuwaita Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah jina la “Wahhaabiyyah”?

Jibu: Sio Wahhaabiyyah. Wao ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Jina bandia la “Wahhaabiyyah” limeanzishwa na maadui ili kuwakimbiza watu kutoka katika Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab. Shaykh hakuja na kitu kutoka kwake mwenyewe. Mwelekeo wake haukuwa mwengine isipokuwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Alikuwa Hanbaliy katika Fiqh, Salafiy katika ´Aqiydah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (81) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-1-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 17/02/2018