Swali: Baadhi ya watu Italia wanasema kuwa Wahhaabiyyah hawampendi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kuwa wanasema kuwa haijuzu kufanya Tawassul kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vipi tutawaraddi?

Jibu: Jibu ni sahali. Tunawaraddi kwa kuwauliza iko wapi dalili ya kwamba mwenye kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatakiwa kutawassul kwake? Anayempenda Mtume anatakiwa kumfuata. Hili ndio linalotakikana. Ama kusema kuwa mtu anatakiwa kufanya Tawassul kwake dalili iko wapi? Atuletee dalili juu ya hili ya kwamba miongoni mwa alama za kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kufanya Tawassul naye. Watuletee dalili juu ya hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (07) http://alfawzan.af.org.sa/node/2122
  • Imechapishwa: 02/07/2020