Wahalifu Kujinasibisha Na Maimamu Wanne Hayawaibishi


Swali: Baadhi ya Suufiyyah wanajinasibisha kwa Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) ambapo baadhi ya watu wakadhania kuwa Imaam ash-Shaafi´iy ana baadhi ya Taswawwuf. Je, hili ni sahihi?

Jibu: Hata siku moja. Imaam ash-Shaafi´iy alipiga vita Taswawwuf. Kitendo cha Suufiy, Mu´tazliy na Ash´ariy kujinasibisha kwake ni kitu kipo. Wengi katika wale wanaofuata madhehebu mane mara nyingi wanakuwa ni katika Ashaa´irah, Mu´tazilah na kadhalika. Kitendo cha kuja wenye kujinasibisha naye baada yake ilihali anafuata madhehebu yanayoenda kinyume na Imaam huyo hakimuabishi. Kuna Hanafiyyah na Shaafi´iyyah wengi wanaoenda kinyume na madhehebu ya maimamu wao Abu Haniyfah na ash-Shaafi´iy. Hali kadhalika Maalikiyyah wana mengi ambayo yanaenda kinyume na aliyokuwemo Imaam Maalik. Hiki ni kitu kipo. Katika mambo ya mataga ni Shaafi´iyyah. Lakini inapokuja katika ´Aqiydah sio Shaafi´iyyah. Vivyo hivyo Hanafiyyah inapokuja katika mambo ya mataga ni Hanafiyyah. Lakini katika ´Aqiydah hawako katika madhehebu ya Abu Haniyfah. Katika Hanaabilah pia kunapatikana watu walio hivyo. Katika mambo ya mataga ni Hanaabilah. Lakini sivyo hivyo inapokuja katika ´Aqiydah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (16) http://alfawzan.af.org.sa/node/2059
  • Imechapishwa: 02/05/2017