Swali: Mtu akiwa na pupa ya kufunga na kuswali katika Ramadhaan peke yake. Lakini anaacha kuswali pale tu ambapo Ramadhaan inakwisha. Je, swawm yake ni sahihi?

Jibu: Swalah ni nguzo moja miongoni mwa nguzo za Uislamu. Nayo ndio nguzo muhimu mno baada ya shahaadah. Swalah ni faradhi kwa kila mtu. Mwenye kuacha kuswali hali ya kuwa anapinga uwajibu wake au kwa sababu ya kuzembea amekufuru.

Kuhusu wale wanaofunga Ramadhaan na wanafunga katika Ramadhaan peke yake huku ni kumhadaa Allaah. Ni uovu wa watu waliyoje ambao hawamtambui Allaah isipokuwa katika Ramadhaan peke yake. Funga zao hazisihi kwa kitendo cha kuacha kwao swalah nje ya Ramadhaan. Bali ni makafiri kwa kitendo hicho. Inahusiana na ukafiri mkubwa. Haijalishi kitu hata kama hawapingi uwajibu wa swalah kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ahadi iliopo baina yetu na wao ni swalah. Yule mwenye kuiacha basi amekufuru.”

Ameipokea Imaam Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwa Buraydah al-Aslamiy (Radhiya Allaahu ´anh).

Pia amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Kichwa cha mambo ni Uislamu, nguzo yake ni swalah na Jihaad katika njia ya Allaah ndio nundu yake ya juu.”[1]

Ameipokea

Ameipokea Imaam at-Tirmidhiy (Rahimahu Allaah) kwa cheni ya wapokezi ambayo ni Swahiyh kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh).

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Baina ya mtu na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”

Ameipokea Imaam Muslim katika ”as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir bin ´Abdillaah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh).

Zipo Hadiyth nyingi zilizopokelewa kwa maana kama hii.

Ibraahiym bin Muhammad Aalush-Shaykh

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

´Abdullaah Maniy´

[1] at-Tirmidhiy (2616) na an-Nasaa´iy (10/214-215) (11330).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (102)
  • Imechapishwa: 24/04/2020