Wafanyakazi wakike leo majumbani wanahesabika ni kama wake?


Swali: Hukumu ya mfanyakazi wa kike nyumbani ni kama hukumu ya mjakazi?

Jibu: Tunamuomba Allaah afya. Wewe mfanyakazi huyu unammiliki? Mjakazi ni mke aliyemilikiwa na mikono ya kiume, amefungishwa mkataba juu yake kwa mikono ya kiume kama mfano wa mkataba wa ndoa. Kwanza wanasema (wanachuoni) kuwa uke uliyomilikiwa na mikono ya kiume una nguvu zaidi kuliko mkataba wa kufunga ndoa. Ama mfanyakazi wa kike huyu hufugunga naye kitu. Huyu ni mfanyakazi tu anakutumikia ambaye amepata ajira. Huyu ni mwajiriwa ambaye ni ajinabi kwako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (51) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-05-27.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014