Wafanya Ruqyah wanachukua msaada kutoka kwa majini waumini


Swali: Baadhi ya wale wenye kufanya matabano wanachukua msaada kutoka kwa majini waislamu dhidi ya majini makafiri…

Jibu: Hapana! Haijuzu kuchukua msaada kutoka kwa majini, wasioonekana wala maiti. Haijuzu kutaka msaada isipokuwa kutoka kwa mtu aliye hai, mbele yako na ambaye ni muweza wa kukusaidia. Ni lazima yapatikane masharti haya:

1- Anatakiwa awe hai na asiwe maiti.

2- Awe mbele yako na asiwe mbali na wewe.

3- Awe ni muweza na asiwe si muweza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (64) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/28-07-1438h-fathou.mp3
  • Imechapishwa: 29/07/2017