Wafanya kazi pia anahitajia Mahram kwenda hajj?


 

Swali: Nina mfanya kazi mwanamke ambaye anataka kuhiji. Je, inajuzu kwake kuhiji na usuhubiano mzuri nikisimamia hajj yake?

Jibu: Hili ni tatizo. Suala hili ni muhimu; wanakusanya wafanya kazi wa kike nyumbani na kuhiji nao. Asli ni kuwa haijuzu kwa mwanamke kusafiri bila ya Mahram:

“Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Vipi iwe msimamo wetu juu ya Hadiyth hii? Vipi tuivuke na tusiitendee kazi? Ili kwenda na desturi za watu? Hapana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_27-07-1433.mp3
  • Imechapishwa: 22/05/2018