Swali: Mimi nina kaka ana umri wa miaka kumi na saba na haswali isipokuwa Ijumaa tu na wakati mwingine haswali hata hiyo Ijumaa haiswali. Unaninasihi nini kuhusiana na yeye? Je, akifa katika hali kama hii ilihali na mimi najua kuwa haswali niwafahamishe watu kuwa hawaswali ili wasimswalie?

Jibu: Ndio, mwenye kuacha Swalah kwa kukusudia ni kafiri. Isipokuwa ikiwa ni mtu ambaye ameondokewa na akili, huyu ´ibaadah sio wajibu kwake. Ama ikiwa yuko na akili na amepitisha miaka ya kubaleghe na anaacha Swalah kwa kukusudia, huyu ni kafiri. Wanasihi watu kwa kuwaambia hali yake ili wasidanganyike naye na wasije wakamswalia na kumzika kwenye makaburi ya Waislamu. Wataamiliane naye kama wanavofanyiwa makafiri [wanapofariki].

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_10.mp3
  • Imechapishwa: 26/06/2018