Waelekezaji na waongozaji wanaoenda hajj kila

Swali: Mimi ni mwanamke ambaye ninahiji kila mwaka. Baadhi ya watu wamenambia kwamba kitendo changu hichi kinawaudhi waislamu kwa njia ya kwamba ninawabana. Pamoja na kukujuza ya kwamba ninawapa faida wale wanawake wanaoenda pamoja nami kwa kuwaelekeza na kuwaongoza. Unasemaje na ni yepi maelekezo yako kwangu? Allaah akujaze kheri.

Jibu: Naona kuwa mwanamke huyu ambaye watu wanafaidika kutoka kwake kwa kuwaelekeza na kuwaongoza afanye hajj. Masuala ya kuwabana, ikiwa hakuwana yeye mwanamke huyu watabanwa na wengine. Lakini mwanamke huyu ana manufa kwa waislamu. Ikiwa yeye ndiye ana jukumu la kuwaongoza na kuwaelekeza wanawake, basi hapana haka kwamba kuhiji kwake ndio bora kuliko kubaki kwake. Ama ikiwa yeye ni kama wanawake wengine, basi hapa tunasema kwamba kumsaidia yule anayetaka kuhiji hajj ya kwanza ambayo ni faradhi ndio bora zaidi. Kwa sababu mtu akimsaidia nduguye kutekeleza ´ibaadah ni kama kwamba yeye mwenyewe ndiye kaifanya. Hivo ndivo alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kumsaidia mwenye kupigana vita basi amepigana vita. Mwenye kumbakilia nafasi yake juu ya familia yake kwa wema basi amepigana vita.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1199
  • Imechapishwa: 16/08/2019