Swali: Nafanya kazi kama afisa wa ndoa. Nimesikia kutoka kwa baadhi ya wanaojinasibisha na elimu kwamba kuwafungisha ndoa wenzi wawili ambapo mmoja wao haswali ndoa hiyo ni batili na kwamba haijuzu kuwafungisha ndoa. Je, ni sahihi? Nikijiwa na watu niulizehali ya wachumba hao kwa upande wa swalah zao au niwafungishe ndoa pasi na kuwauliza?

Jibu: Ukijua kuwa mmoja katika wachumba hao haswali basi usimfungishe ndoa kwa huyo mwingine. Kuacha swalah ni ukafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Baina ya mtu na shirki na ukafiri ni kuacha swalah.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

 Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema tena:

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule atakayeiacha amekufuru.”

Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa nne wa Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Tunamuomba Allaah azitengeneze hali ya waislamu na awaongoze wapotofu katika wao. Kwani hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Aliye karibu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/396)
  • Imechapishwa: 30/06/2021