Wachawi wanamtisha aache matabano


Swali: Mimi ni msomaji Ruqyah ambaye ninawasomea wahitaji na wagonjwa na sipokei pesa hata moja. Ninachotaka ni ujira kutoka kwa Allaah na ninamuomba anikubalie kitendo changu. Nimejiwa na wachawi na mashaytwaan ambao wamenitisha na kuniudhi mimi na familia yangu. Je, niache Ruqyah kwa ajili ya jambo hili. Unaninasihi nini?

Jibu: Mtegemee Allaah na usiache Ruqyah. Usiache Ruqyah na usitishike na vitisho vyao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (44) http://alfawzan.af.org.sa/node/2150
  • Imechapishwa: 06/09/2020