Wacha yashughulikiwe na wanachuoni na usiwe na kiherehere

Kulingania na kurekebisha hakuwi namna hiyo; uchochezi, porojo nyingi na kuwahamasisha vijana.

Hayo ndio niliyosema, na ndio ninayosema hivi sasa na baada ya hivi sasa: Ambaye anatakiwa kuraddi na kujadili ni Shaykh. Shaykh mpaka sasa bado yuko hai. Hivyo basi, tunawanasihi vijana wasijiingize katika yale yanayopitika kati ya wanafunzi na wanachuoni. Shaykh akimtia makosani Shaykh mwingine, basi Shaykh ndiye ambaye anatakiwa kuraddi. Ni kwa nini wewe unataka kujichosha? Ni kipi utafaidika ukijiingiza kati ya wanachuoni? Hakuna jengine isipokuwa tu kutumbukia katika usengenyi na kuwasema vibaya wanachuoni na wanafunzi – hukufaidika chochote. Bali umekhasirika. Kwa ajili hiyo tunawanasihi vijana wetu wajiepushe na msimamo huo usioendana nao.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Amaan bin ´Aliy al-Jaamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=MkpDU1ftzfs&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 17/01/2021