Vyamavyama na makundi mbalimbali hayana lolote kuhusiana na Uislamu


Swali 195: Ni ipi hukumu ya Shari´ah juu ya uwepo wa makundi mengi na mapote na mitandao pamoja na kwamba ni yenye kutofautiana kati yake katika mifumo yake, njia zake, Da´wah zao, ´Aqiydah zao na misingi iliosimama juu yake na khaswa ukizingatia kwamba kundi la haki ni moja, kama ilivyojulisha hivo Hadiyth?

Jibu: Haifichikani kwa kila muislamu ambaye ni mtambuzi wa Qur-aan na Sunnah na yale waliyokuwemo juu yake wema wetu waliotangulia ya kwamba vyamavyama na makundi ni yenye kutofautiana katika fikira kwanza na pili njia zao. Kwa hivyo hayana chochote kuhusiana na Uislamu. Bali ni jambo ambalo Mola wetu (´Azza wa Jall) amelikataza katika Aayah nyingi za Qur-aan kama mfano wa pale aliposema (Ta´ala):

وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

“… na wala msiwe miongoni mwa washirikina; miongoni mwa wale walioifarikisha dini yao wakawa makundimakundi – kila kundi wananafurahia waliyonayo.”[1]

Hapana shaka yoyote kwamba kundi lolote linalotaka kwa pupa yake kufikisha na kumtakasia Allaah (´Azza wa Jall) basi wawe katika Ummah uliorehemewa, hakika hakuna njia ya kufikia jambo hilo na kuhakikisha kwa kimatendo katika jamii za Kiislamu isipokuwa kwa kurejea katika Qur-aan na Sunnah na yale waliyokuwemo watangu wetu wema (Radhiya Allaahu ´anhum).

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameweka wazi mfumo na njia iliosalimika kwa yeye siku moja kupiga juu ya ardhi msitari ulionyooka kisha akapiga pembezoni mwake vijia vifupivifupi kando na njia ile ilionyooka. Hapana shaka kwamba vijia hivi vifupi ndivo vinavowakilishwa na vyamavyama na makundi haya mengi. Kwa ajili hiyo ndio maana ni wajibu kwa kila muislamu apupie awe – tena kwa haki – katika kundi lililookoka na afuate njia ilionyooka na asende kuliani wala kushotoni. Ndio maana miongoni mwa alama za kundi lililookoka ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amelibainisha wakati alipoulizwa juu yake ambapo akasema:

“Ni lile litalofuata yale ninayofuata mimi na Maswahabah zangu.”

[1] 30:31-32

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 408
  • Imechapishwa: 17/02/2020