Vyakula vya Ahl-ul-Kitaab vinavyoandikwa “haina-pombe”, “haina-nguruwe”


Swali: Baadhi ya migahawa na vinywaji vinaandikwa “haina-nguruwe”, au “haina-pombe”. Je, mtu atosheke na maandiko kama haya na kuvitumiaau kuna neno?

Jibu: Hakuna neno, maandiko haya yanatosha ikiwa ni katika mji wa mayahudi na manaswara, yanatosha maandiko haya. Asli ni kuwa, chakula (vichinjo) vyao ni Halali hata kama hakikuandikwa kitu. Na ikiwa kimeandikwa, inakuwa ni aula zaidi. Isipokuwa tu ikijulikana ya kuwa haya (waliyoyaandika) ni uongo na katika kitu hichi kuna nguruwe au kuna kitu kingine cha najisi, maandiko haya yatakuwa hayana maana yoyote. Ikijulikana kwa dalili kutoka kwa waaminifu ya kwamba, huu ni uongo. Ama maadamu hakujajulikana kitu, asli ni kwamba inaruhusu na ni salama.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 31/03/2018