Swali: Pindi mtu anapokataza maovu kuna baadhi ya watu wanaosema mtu awaachie viumbe Muumba. Je, ni sahihi?

Jibu: Hapana. Haijuzu kusema hivo. Maovu yanatakiwa kukemewa na kubainishwa kwa watu. Haitakiwi kusema waachwe viumbe kwa Muumba. Waachwe wafanye watakavyo ili Allaah awahesabu? Hapana, ni wajibu wako kuamrisha mema, kukataza maovu na kulingania kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (66) http://alfawzan.af.org.sa/node/16524
  • Imechapishwa: 13/08/2017