Vitu vyenye kutia shaka na visivyotia shaka

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

11- Abu Muhammad al-Hasan bin ‘Aliy bin Abiy Twaalib mjukuu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kipenzi chao (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Nilihifadhi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yafuatayo: “Wacha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka.”

Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

“Achana na kile chenye kukutia shaka… “

Bi maana kitu kimoja chenye kukutia shaka.

“… na ufuate vitu elfu nne visivyokutia shaka.”

Anachomaanisha kwa kusema hivo ni kwamba, vyenye kutia shaka ni vitu vichache mno na visivyotia mtu shaka, sawa katika maneno, matendo au mambo ya imani, ni vitu vingi mno. Himdi zote anastahiki Allaah.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 205
  • Imechapishwa: 15/05/2020