Swali: Ni ipi hukumu kuswali na kucha refu?

Jibu: Kwa hali yoyote haitakikani kubakiza kucha refu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuzikata na amri inapelekea katika ulazima. Ni lazima kukata kucha, masharubu na kunyofoa nywele za kwapani. Imethibiti katika Hadiyth Swahiyh isemayo:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituwekea muda wa kukata kucha, kupunguza masharubu, kunyofoa nywele za kwapani na kunyoa nywele za sehemu ya siri kwamba tusiache chochote katika hivyo zaidi ya nyusiku arobaini.”

Kwa hiyo haitakikani kwa muislamu kuziacha zaidi ya nyusiku arobaini. Bali Sunnah ni kukata masharubu kabla ya siku hizo, vivyo hivyo kukata kucha kwa mwanamme na mwanamke, kunyofoa nywele za kwapani kwa mwanamme na mwanamke na vivyo hivyo kunyoa nywele za sehemu ya siri kwa mwanamme na mwanamke. Yote haya yanatakiwa kuharakishwa na kupatilizwa kabla ya nyusiku arobaini. Mwanamme apunguze masharubu yake, akate kucha zake, anyofoe nywele zake za kwapani na anyoe nywele zake za sehemu ya siri. Hali kadhalika mwanamke akate kucha chake, anyofoe nywele zake za kwapani na anyoe nywele zake za sehemu ya siri kwa kutumia baadhi ya dawa kama anavofanya mwanamme. Hii ni Sunnah iliyokokotezawa. Pengine ikasemwa kuwa ni lazima. Kwa sababu ametupangia muda tusiziache zikazidi nyusiku arobaini. Amri ya kupunguza masharubu, kukata kucha na kunyofoa nywele za kwapani imetoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Udhahiri wa mambo haya ni lazima na kwamba haijuzu kuyaacha kwa njia ya hali kuonekana vibaya na ikazingatiwa kuwa ni ndefu kidesturi. Kitendo hichi kinaenda kinyume na Sunnah iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yale yanayofanywa na baadhi ya watu ambapo wanarefusha kucha ni maovu yasiyokuwa na msingi na kuwaiga baadhi ya maadui wa Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/5359/حكم-اطالة-المراة-اظفارها
  • Imechapishwa: 18/04/2022