Vitenguzi vya Uislamu ndio vitenguzi vya imani

Swali: Je, kuna tofauti kati ya vitenguzi vya Uislamu na vitenguzi vya imani?

Jibu: Hapana, hakuna tofauti. Vitenguzi vya Uislamu ndio vitenguzi vya imani. Lakini mtu anaweza kuwa muislamu kwa ulimi wake tu na wakati huohuo akawa mnafiki. Amesema (Ta´ala):

وَلَقَدْ قَالُوا كَلِمَةَ الْكُفْرِ وَكَفَرُوا بَعْدَ إِسْلَامِهِمْ

”… na hali wamekwishasema neno la kufuru na wakakufuru baada ya Uislamu wao.” (at-Tawbah 09:74)

Amesema kuhusu waumini:

لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Hivyo msitoe udhuru, kwani mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (at-Tawbah 09 : 65-66)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 30
  • Imechapishwa: 15/11/2019