Vitabu vinavyotakiwa kusomwa Ramadhaan

Swali: Ni vitabu vipi unavyotupendekezea kusoma katika Ramadhaan?

Jibu: Soma Aayah za Qur-aan na Hadiyth zenye kuzungumzia juu ya swawm na fadhila za swawm. Ikiwa uko na upeo wa elimu wa kuweza kuwafasiria nazo watu, fanya hivo. Vinginevyo inatosheleza kwako kuwasomea watu. Wasomee watu Aayah za Qur-aan na Hadiyth huku wasikilize.

Kuna vitabu vilivyoandikwa kwa ajili ya Ramadhaan. Kwa mfano “Latwaa´if-ul-Ma´aariyf” cha Ibn Qaasim kifupi. Ni kitabu kifupi na kizuri. Kina faida kubwa. Asiyekuwa na elimu akisome na awasomee watu kwa sababu ni kitabu aminifu na chenye faida. Kadhalika kitabu “al-Lu´lu´ wal-Marjaan fiy Wadhwaa´if Shahr Ramadhwaan” cha Shaykh wetu Ibraahiym bin ´Ubayd Aal ´Abdil-Muhsin. Ni kitabu chenye manufaa na kina faida nyingi. Asome ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-10-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020