Swali: Ni vitabu vipi unavyopendekeza na ni vitabu vipi unavyotahadharisha?

Jibu: Napendekeza Qur-aan, Sunnah na vitabu vyote vya Salaf, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa jumla. Havihesabiki. Atakayevifanya ni vyanzo juu ya dini na elimu yake atatosheka navyo. Hahitajii vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah.

Tunatahadharisha vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal; vitabu vya Suufiyyah, vitabu vya Khawaarij, vitabu vya Raafidhwah, vitabu vya al-Ikhwaan al-Muslimuun, vitabu vya Qutbiyyuun. Vyote hivi ni vitabu vya Bid´ah na upotevu. Tunawatahadharisha vijana wa Ummah navyo. Vivyo hivyo inahusiana na mikanda ya watu hawa inayoenda kinyume na mfumo wa Salaf. Anayetaka kulelewa juu ya mfumo wa Allaah wa haki na mfumo wa Salaf basi atambue kuwa vyanzo vyake vimejaa. Uhai wote wa mtu unaweza kwenda na mtu asijaaliwe kuvipitia vyote.

Ni kipi kinachomvutia na vitabu vya wapotevu? Tangu ile siku ya kwanza ataanza kufuata vitabu vya wapotevu. Hoja yake ni kuwa anaweza kupambanua kati ya haki na batili; anadai kuwa anachukua yale ambayo ni haki na anaacha yale ambayo ni batili. Mwishowe anachukua yale ambayo ni batili na anaacha yale ambayo ni haki. Haya yamewapitikia watu wengi.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf-us-Sitaar, uk. 20
  • Imechapishwa: 06/11/2016