Swali: Ni vitabu vipi vinavobainisha mifumo kama ya Qadariyyah, Jahmiyyah, Khawaarij, Mu´tazilah na wengine? Ni kitabu kipi bora katika mada hii?

Jibu: Mimi sipendelei kwenu msome mambo haya. Ninachelea juu yenu. Ni sawa tu kwa mtu ambaye yuko imara katika elimu na maarifa. Mwanafunzi anayeanza asisome fikira kama hizi. Kuna vitabu vingi vilivyoandikwa juu ya mada hii. Ibn Hazm ana kitabu kinachoitwa “al-Fiswal fiyl-Milal wan-Nihal”, “ash-Shihristwaaniy ana kitabu kinachoitwa “al-Milal wan-Nihal”, “Abul-Hasan al-Ash´ariy ana kitabu kinachoitwa “Maqaalaat-ul-Islaamiyyiyn” na [´Abdul-Qaahir] al-Baghdaadiy ana kitabu kinachoitwa “al-Farq bayn al-Firaq”. Vyote hivi vinahusu mapote na madhehebu na vimechapishwa. Lakini pamoja na hivyo sipendelei kuvisoma mpaka pale mtapokuwa imara kweli kweli katika elimu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–02041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015