Kitu kinachompambanua muislamu wa kweli na mwerevu ni kwamba ana imani sahihi na ya kweli kwa yale yaliyomo katika Qur-aan na Sunnah, anajisalimisha nayo na kujiepusha kupinda kwayo, kuyapotosha au kurudisha kitu katika hayo.

Mambo haya ya khatari hufanywa na Ahl-ul-Ahwaa´ sawa wale wanaotumbukia katika upindukaji na wale wenye kuzembea. Katika sampuli mbili ya watu hawa wako ambao wamejificha nyuma ya Salafiyyah na wanadai kuwa wao ndio Ahl-ul-Hadiyth ilihali uhakika wa mambo wako mbali kabisa na mfumo wa Salaf na Ahl-ul-Hadiyth. Bali hakuna watu wanaowapiga vita Salafiyyuun kama wanavyofanya wao.

Katika wao kuna Haddaadiyyah Qutbiyyah ambao wanawapiga vita Ahl-ul-Hadiyth was-Sunnah. Pindi wanapowatuhumu Ahl-us-Sunnah kwa Irjaa´ matokeo yao ni fikira za Mahmuud al-Haddaad (ambaye alikuwa ni Qutbiy mwenye kujificha), Muhammad Qutwub na mwanafunzi wake Safar al-Hawaaliy.

Muhammad Qutwub ametuhumu jamii ya Kiislamu ya kale na iliyokuja baadae kuwa na Irjaa´ na kudai kuwa Irjaa´ ni mbaya zaidi kuliko uanasekula.

Kwa ajili ya kutilia nguvu fikira hii mwanafunzi wake Safar al-Hawaaliy akazusha kanuni ya khatari inayoitwa “Jins-ul-´Amal”[1].

Pamoja na misingi mingine Haddaadiyyah Qutbiyyah wanazungumza kwa fikira hii ya khatari na misingi ya batili kwa ajili ya kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah wat-Tawhiyd. Kazi yao kubwa ni kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah wat-Tawhiyd. Wanafanyia kazi unafiki kwa sababu ya udanganyifu na njama ili kuwapaka watu na hata baadhi ya wanachuoni mchanga wa machoni. Khaswa khaswa mbele ya wanachuoni wanajionyesha kuwa ni wenye kushikamana na mfumo wa Salaf na kuwa na ghera juu yake ilihali uhakika wa mambo ni kwamba ni katika Ahl-ul-Ahwaa´ wenye kuwapiga vita vikali na kuuchafua vibaya mfumo wa Salaf na Salafiyyuun.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/neno-jins-ul-amal-limetoka-kwa-murji-ah/

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=287
  • Imechapishwa: 09/10/2016