Vipindi vya redio vinavyotiwa muziki


Swali: Ni ipi hukumu ya kusikiliza baadhi ya barnamiji zenye faida kama mfano wa vipindi vya magazeti na mfano wake vinavyoingiliwa na muziki?

Jibu: Hapana neno kusikiliza na kufaidika pamoja na kufunga redio pale tu muziki unapoanza mpaka utakapomalizika. Muziki ni katika jumla ya zana za pumbao. Allaah afanye wepesi kuiacha na kusalimika kutokamana na shari yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/490)
  • Imechapishwa: 06/03/2021