Vipindi vya Da´wah vilivyoanzishwa na Jamaa´t-ut-Tabliygh ni Bid´ah

Swali: Je, kuwalazimisha watu kutoka kulingania kwa kipindi cha siku nne, mwezi mzima na miezi minne ni katika kujikakama kunakosimangwa au ni kufanya bidii katika mambo ya kheri?

Jibu: Ni katika Bid´ah. Mambo haya hayaitwi kuwa ni kujikakama kunakosimangwa peke yake, isipokuwa Bid´ah pia. Hizi ni miongoni mwa Bid´ah za Suufiyyah. Da´wah haina kikomo cha siku maalum, miezi minne na kadhalika. Yote haya ni katika Bid´ah ambazo Allaah hakuziteremshia dalili yoyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/bryhari–1427-10-7.mp3 Tarehe: 1427-10-07/2006-10-30
  • Imechapishwa: 26/05/2022