Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia wanja na vipodozi kwa wanawake mchana wa Ramadhaan? Je, vinafunguza?

Jibu: Wanja hauwafunguzi wanawake wala wanaume kabisa kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Lakini kuutumia usiku ndio bora zaidi kwa mfungaji. Kadhalika vile vitu vya kusafisha uso kama vile sabuni, mafuta na vyenginevyo vinavyowekwa juu ya ngozi. Katika hayo kunaingia vilevile hina, vipodozi na mfano wake. Vyote hivyo vina neno kwa mfungaji. Pamoja na kwamba haitakiwi kutumia vipodozi ikiwa vinadhuru uso.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/259-260 )
  • Imechapishwa: 26/05/2018