Vipi swawm ya ambaye hakuweza kuamka kula daku?


Swali: Kuna mtu alilala kabla ya kula daku katika Ramadhaan na alikuwa na nia ya kuamka kula daku. Akashtukiza amelala mpaka asubuhi. Je, swawm yake ni sahihi?

Jibu: Swawm yake ni sahihi. Daku sio sharti ya kusihi kwa swawm. Daku imependekezwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuleni daku. Hakika katika kula daku kuna baraka.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

[1] al-Bukhaariy (1923) na Muslim (1095).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/321)
  • Imechapishwa: 02/06/2018