Vipi swawm ya ambaye amepata hedhi punde tu baada ya jua kuzama?


Swali: Ni ipi hukumu ya swawm ya mwanamke akipata hedhi muda kidogo baada ya jua kuzama?

Jibu: Swahiyh yake ni sahihi. Hata kama atahisi alama ya kupata hedhi kabla ya jua kuzama, kama vile maumivu, lakini asiione yenye kutoka isipokuwa baada ya jua kuzama. Katika hali hiyo swawm yake ni sahihi. Kwa sababu kitu kinachoharibu swawm ni damu ya hedhi na sio yale maumivu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/192)
  • Imechapishwa: 18/05/2018