Vipi swawm ya ambaye amepata hedhi kabla ya futari na kabla ya kuswali Maghrib?


Swali: Ni wajibu kulipa swawm mwanamke akipata ada yake ya mwezi baada ya swalah ya Maghrib au kabla ya swalah baada ya kufuturu?

Jibu: Hatakiwi kulipa akikamilisha swawm kisha akapata hedhi baada ya jua kuzama ijapokuwa ni kabla ya swalah. Hakuna neno kwake. Vivyo hivyo ikiwa ni baada ya swalah, jambo ambalo lina haki zaidi ya kutolipa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/192)
  • Imechapishwa: 18/05/2018