Vipi mwanamke mwenye hedhi akisafika mchana wa Ramadhaan?

Swali: Ni ipi hukumu mwenye hedhi akisafika katikati ya mchana wa Ramadhaan?

Jibu: Ni lazima kwake kujizuia [kula, kunywa n.k.] kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Kwa sababu ameondokewa na udhuru wa Kishari´ah. Vilevile itakuwa ni wajibu kwake kuilipa siku hiyo. Kama ambavyo ikithibiti kuonekana mwezi mwandamo mchana wa Ramadhaan, basi katika hali hiyo waislamu wanatakiwa kujizuia siku iliyobaki na kuilipa siku hiyo kwa mujibu wa mtazamo wa wanachuoni wengi. Mfano wake ni msafiri akifika katika mji wake mchana wa Ramadhaan basi ni lazima kwake kujizuia kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Kwa sababu hukumu ya safari kwake imeshaondoka. Hata hivyo anatakiwa kuilipa siku hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/193)
  • Imechapishwa: 19/05/2018