Vipi mtu atamsusa mwanamke muasi chumbani?


Swali: Umetaja maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ

“Wahameni katika malazi.” (04:34)

Je, ina maana ya kwamba mtu ajitenge mbali na kitanda chake au mtu alale naye bila ya kuongea naye na kufanya naye jimaa?

Jibu: Aayah ni kwa jumla. Ni pamoja na kwamba analala kwenye kitanda kimoja naye bila ya kuongea naye na kustarehe naye na kwamba analala sehemu nyingine. Nimetaja sehemu ya mwisho na kwamba analala sehemu nyingine kama kwenye chumba kingine, katika nyumba nyingine na kadhalika. Makusudio ni kwamba afanye kile ambacho anaonelea [kuwa ni sawa] ili aweze kumfanya kuwa bora.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (21)
  • Imechapishwa: 20/09/2020