Ukishajua madhehebu ya Khawaarij kwamba msingi wao ni kukufurisha kwa madhambi na wakawakufurisha Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakahalalisha kuwaua hali ya kuwa ni wenye kujikurubisha kwa Allaah. Ukishabainikiwa na hayo basi utabainikiwa na upotevu wa watu wengi wa zama hizi ambao wanadai kwamba Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na wafuasi wake kwamba ni Khawaarij. Uhakika wa mambo ni kwamba madhehebu yao ni kinyume na madhehebu ya Khawaarij. Kwa sababu wao wanawapenda Maswahabah wote wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanaamini kuwa wao ni bora kuliko wale waliokuja baada yao. Wanayawajibisha hayo wale wafuasi wao, wanawaombea du´aa, wanamtia katika upotevu yule anayewaponda au kumtukana mmoja katika wao. Hawakufurishi kwa madhambi. Hawawatoi watenda madhambi nje ya Uislamu.

Wanamkufurisha yule mwenye kumshirikisha Allaah na akaifanya shirki kuwa nzuri. Mshirikina ni kafiri kwa mujibu wa Qur-aan, Sunnah na maafikiano. Vipi basi hawa watafananishwa na hawa wengine? Hakuna mwengine anayesema hayo isipokuwa yule ambaye ni mkaidi malengo yake ni kuwafanya wale watu wa kawaida wakimbie, anasema hivo akiwa ni mjinga juu ya madhehebu ya Khawaarij au hali ya kufuata kichwa mchunga.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan Abaa Butwayn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Rasaa-il wal-Masaa-il an-Najdiyyah (02/176)
  • Imechapishwa: 18/03/2019