Swali: Vipi mwanamke anatakiwa kujisitirina Hijaab? ? Je, ni mwili wake wote? Je anaweza kuonesha vitanga vyake vya mikono na uso wake kwa Mahram zake wote?

Jibu: Mwanamke anatakiwa kujisitiri kwa watu ambao sio Mahram zake; jirani yake, watoto wa ami yake, mume wa kaka yake. Ama Mahram zake si lazima awe na na Hijaab; hakuna neno akaonesha uso wake, vitanga vyake na miguu yake kwa Mahram zake; kama kaka yake, ami yake na yake, hakuna ubaya. Muhimu ni yeye kujisitiri mbele ya watu ajinabi; kama kwa mfano mtoto wa mjomba wake, kwa kuwa ni ajinabi kwake na sio Mahram. Na kama kwa mfano mume wa dada yake, kaka wa mume wake, ami wa mume wake na mfano wa hawa. Watu hawa ni juu yake kujisitiri mbele yao mwili wote; kuanzia uso mpaka chini. Kwa Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ

“Na mnapowauliza (wake zake) haja, waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.” (33:53)

Anasema tena (Subhaanah):

وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ

“Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao… ” (24:31)

Hivyo ni kuwa, kaamrishwa kujisitiri kwa Hijaab kwa watu ambao sio Mahram zake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb (770)
  • Imechapishwa: 12/03/2018