Swali: Ikiwa baadhi ya watu wanaenda kinyume na Sunnah ni lazima kwetu kuwanasihi? Mtu anawanasihi vipi?

Jibu: Unatakiwa kuwanasihi kwa upole na uwafunze. Ukimuona anavaa nguo chini ya kongo mbili za miguu unatakiwa kumnasihi. Ukimuona harambi vidole vyake [baada ya kumaliza kula] unatakiwa kumfunza. Unamuona anakula kwa mkono wa kushoto unatakiwa kumfunza. Ukimuona anafanya mambo mengine yasiyokubalika katika Shari´ah unatakiwa kumnasihi. Lakini unatakiwa ufanye hivo kwa kuzungumza maneno mazuri na njia nzuri. Mola wetu (´Azza wa Jall) amesema:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.”[1]

Swali: Nasaha inakuwa kwa siri au hadharani?

Jibu: Kutegemea na hali. Ikiwa ni mbele za watu mnasihi kati yako wewe na yeye. Na ikiwa ni kati yako wewe na yeye basi nyanyua sauti yako. Na ikiwa ni mbele za watu mwambie kwa siri ili isiwe sababu ya kurudisha nyuma nasaha na akubali nasaha.

[1] 16:125

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21519/ما-كيفية-التعامل-مع-من-يخالفون-السنة
  • Imechapishwa: 24/08/2022