Vipi kunakuwa kujishusha (التواضع)?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth:

“Allaah ameniteremshia Wahy nijishushe ili asijifakharishe yeyote juu ya mwingine na asimdhulumu yeyote juu ya mwingine.”

Ni vipi kunakuwa kujishusha katika hali hii?

Jibu: Uhakika wa kujishusha ni wewe kutangamana na wengine vile unavopenda watangamana nawe na utangamane nao kama mmoja katika ndugu zao. Udugu wa imani ndio uliokukusanyeni. Kwa hivyo utapojiweka chini mbele yake hutojifakhari mbele yake kwa nasaba yako. Usiseme kuwa yeye ana nasaba duni kuliko wewe na kwamba unajifakhari juu yake kwa sababu ni mtukufu na mengineyo. Usijifakhari kwa nasaba yako, pesa zako, cheo chako na wala usimdhulumu kimabavu kwa ukadai kuwa wewe una haki zaidi kuliko yeye kwa mambo mengi na kwamba yeye hastahiki kitu. Hapana. Ni ndugu yako. Tahadhari usijivune mbele yake, ukamdhulumu na kumshambulia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/كيف-يكون-التواضع
  • Imechapishwa: 19/06/2022