Vipi kuhusu swawm ya mwanamke mjamzito?

Swali: Katika mwezi wa Ramadhaan mtukufu nilikuwa mjamzito na siku ishirini za Ramadhaan nilikuwa msafi ambapo nikafunga na nikala siku nne nikiwa hospitalini. Baada ya Ramadhaan nikalipa zile siku nilizokula. Vipi kuhusu swawm yangu niliyolipa ilihali mtoto akiwa tumboni mwangu?

Jibu: Funga yako ukiwa mjamzito na wakati huo huo ukiwa msafi haiathiri swawm yako. Ni kama swawm ya mwanamke mwenye damu ya ugonjwa. Kwa hivyo swawm yako ni sahihi. Yale masiku mane uliyokula ukiwa hospitalini kisha ukayalipa baada ya  Ramadhaan yanatosha na wala haikulazimu kuyafunga kwa mara nyingine.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/225)
  • Imechapishwa: 10/06/2017