Swali 416: Kutoka kwa damu kwenye fizi za aliyefunga kunamuharibia swawm?

Jibu: Damu inayotoka kwenye meno haiathiri funga. Lakini ajitahidi kutoimeza kiasi na anavyoweza. Kadhalika iwapo atatokwa na damu puani na akajitahidi kutoimeza. Hakuna kitu katika hilo na wala haimlazimu kuilipa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 476
  • Imechapishwa: 09/05/2019