Vipi itajuzu kuwaoa mayahudi?


Swali: Vipi mayahudi watakuwa ni wenye uadui mkubwa kwa waumini pamoja na hivo iwe ni jambo lenye kuwezekana kuoa kwao?

Jibu: Hili ni jambo limewekwa katika Shari´ah na Allaah (´Azza wa Jalla). Hii ni Shari´ah ya Allaah kwa kuwa wanaamini Manabii kwa jumla na vitabu. Wao sio kama waabudu masanamu ambao hawamwamini Nabii wala kitabu chochote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (48) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-04-15.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014