Swali: Ni ipi hukumu kwa mlinganizi anayesema kuwa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayakubaliwi isipokuwa kwa dalili?
Jibu: Huyu vipi atakuwa ni mlinganizi? Mlinganizi hawi isipokuwa yule ambaye ana elimu ya Kishari´ah. Ama kuhusu huyu ni mjinga au ni mkaidi. Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio dalili yenyewe:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

“Na lolote lile analokupeni Mtume, basi lichukueni; na lolote lile analokukatazeni, basi liacheni.” (59:07)

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

“Na wala hatamki kwa matamanio yake. Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa kwake.” (53:03)

Dalili kwanza ni Qur-aan, kisha kunakuja Hadiyth Swahiyh, kisha kunakuja Ijmaa´ halafu ndio kunakuja kipimo sahihi. Hii ndio misingi ya dalili. Lakini huyu hajui. Ima ni mjinga, na ni vipi atakuwa ni mlinganizi? Au ni mkaidi – tunaomba kinga kwa Allaah – na mpotevu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus al-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14759
  • Imechapishwa: 17/01/2017