Vipi Hawa Waweze Kufanya Haya Na Wanachuoni Wakubwa Wasiyaweze?

Swali: Kuna wanachuoni wengi wakubwa ambao hakukudhihiri kwao karama…

Jibu: Sio lazima. Abu Bakr hakukudhihiri kwake karama. ´Umar hakukudhihiri kwake karama. Sio lazima walii kudhihiri kwake karama. Karama hudhihiri pale zinapohitajika. Katika hali hii ndio hudhihiri. Ama ikiwa hazihitajiki sio lazima kila walii kudhihiri kwake karama. Miongoni mwa masharti ya walii sio lazima awe na karama.

Swali: … na kuna waliopindukia katika ´ibaadah ambao wamejishughulisha na ´ibaadah na kumedhihiri kwao karama.

Jibu: Mmeshaambiwa kuwa yule ambaye kutadhihiri kwake mambo yasiyokuwa ya kawaida ilihali sio mfanya ´ibaadah, basi ayafanyayo ni mambo ya kishaytwaan. Mfano wa watu hawa ni wachawi, makuhani na wanajimu. Watu kama hawa hudhihiri kwao mambo yasiyokuwa ya kawaida. Mashaytwaan huwafanyisha mambo kama kuwarukisha angani, wakatembea juu ya bahari, wakatembea juu ya moto na mambo mengine. Haya ni matendo ya kishaytwaan na sio karama.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 29/11/2016