Vipi hajj ya mwanamke ambaye amepoteana na mumewe?

Swali: Mwaka uliyopita nilihiji mimi na mume wangu. Siku ya ´Arafah mume wangu alipoteana nami na hatukuonana isipokuwa baada ya kumalizika hajj nchini kwetu. Je, hajj yangu ni sahihi au ni pungufu?

Jibu: Hajj ni sahihi. Haina upungufu wowote. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

”Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[2]

Afanye nini akimkosa mume wake? Aendelee kufanya hajj yake na arudi pamoja na marafiki zake.

[1] 64:16

[2] 02:286

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1427
  • Imechapishwa: 07/07/2020