Swali: Baadhi ya wanafunzi wanasema kuwa haijuzu kutumia vipasa sauti wakati wa swalah.

Jibu: Waulizeni dalili. Vipasa sauti vinatumiwa ili watu wasikie. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumia mtu ili afikishe sauti. Ni ala inayofikisha. Ni neema kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Lakini tunaona jinsi baadhi ya maimamu wanavyopitiliza kunyanyua sauti kwa kiasi cha kwamba inawaudhi hata maamuma nyuma yake. Sauti inatakiwa iwe ya wastani. Hakuna haja ya kunyanyua sauti kiasi hicho. Lengo ni waswalaji wasikie. Inatosheleza wao kusikia. Nyanyua sauti kiasi cha wao kusikia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_27-07-1433.mp3
  • Imechapishwa: 23/05/2018