Vilivyo vya halali winamtosheleza mwanadamu   

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

30- Abu Tha’labah al-Khushaniy Jurthuum bin Naashir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) amefaridhisha faradhi basi msiyapuuze. Vilevile akaweka mipaka msiivuke. Ameharamisha baadhi ya mambo kwa hivyo usifanye. Kuhusu yale aliyoyanyamazia ni kwa ajili ya huruma Yake kwenu – na si kwamba ameyasahau – kwa hivyo usiyadadisi.”

Shari´ah haikukataza kitu kilicho na manufaa kwa mwanaadamu katika maisha yake. Kila kilicho cha haramu mtu anaweza kujitosheleza nacho na hilo lisimuathiri kitu katika maisha yake. Aliyoharamisha Allaah (Jalla wa ´Alaa) au Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) miongoni mwa vitu, mwanaadamu hana haja nayo ili kuweza kuyasimamisha maisha yake au kuyastarehesha maisha yake. Hakika mtu anaweza kujistarehesha na vingi vilivyohalalishwa na kupendekezwa ambavyo vinamtosheleza na ya haramu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 423
  • Imechapishwa: 13/05/2020