Vijana wasioweza kuoa kwa sababu ya ukubwa wa mahari

Swali: Ni ipi hukumu ya kijana ambaye amekataa kuoa kwa sababu ya mahari kuwa juu na kutokuwa na uwezo wa kuhudumia?

Jibu: Yule ambaye hali yake ni kama ilivyotajwa ambapo hakuna uwezo wa mahari na kuhudumia basi ni mwenye kupewa udhuru. Ni lazima kwake kufunga ili aweze kuihifadhi tupu yake kutokamana na machafu. Akiwa ana uwezo wa mahari na kuhudumia na akakataa kuoa basi ni mwenye kwenda kinyume na Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Enyi kongamano la vijana! Yule atakayeweza miongoni mwenu kuoa basi na aoe. Hakika hilo linamfanya ainamishe macho na inahifadhi utupu wake. Yule asiyeweza basi ni juu yake afunge. Kwani kwake ni kinga.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] al-Bukhaariy (1905), Muslim (1400), at-Tirmidhiy (1081) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (18/23-24)
  • Imechapishwa: 20/08/2017